Jeremiah 20:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, utajiri wote wa mji, mapato yake yote, vitu vyake vyote vya thamani pamoja na hazina zote za wafalme wa Yuda, nitazitia mikononi mwa maadui zao ambao watazipora na kuchukua kila kitu hadi Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mali zote za mji huu, na mapato yake yote, na vitu vyake vya thamani vyote pia, naam, hazina zote za wafalme wa Yuda, nitavitia katika mikono ya adui zao, watakaowateka nyara, na kuwakamata, na kuwachukua mpaka Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, utajiri wote wa mji, mapato yake yote, vitu vyake vyote vya thamani pamoja na hazina zote za wafalme wa Yuda, nitazitia mikononi mwa maadui zao ambao watazipora na kuchukua kila kitu hadi Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao, yaani, mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mali zote za mji huu, na mapato yake yote, na vitu vyake vya thamani vyote pia, naam, hazina zote za wafalme wa Yuda, nitavitia katika mikono ya adui zao, watakaowateka nyara, na kuwakamata, na kuwachukua mpaka Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, utajiri wote wa mji, mapato yake yote, vitu vyake vyote vya thamani pamoja na hazina zote za wafalme wa Yuda, nitazitia mikononi mwa maadui zao ambao watazipora na kuchukua kila kitu hadi Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo mali zote za mji huu nitazitoa, na mapato yao yote na vitu vyao vyote vyenye kiasi kikubwa na vilimbiko vyote vya mfalme wa Yuda, nitavitia mikononi mwa adui zao, wavipokonye, wavichukue na kuvipeleka Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mali zote za mji huu, na mapato yake yote, na vitu vyake vya thamani vyote pia, naam, hazina zote za wafalme wa Yuda, nitavitia katika mikono ya adui zao, watakaowateka nyara, na kuwakamata, na kuwachukua mpaka Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya hiyo, utajiri wote wa muji, mapato yake yote, vitu vyake vyote vya bei kali pamoja na akiba zote za wafalme wa Yuda, nitavitoa katika mikono ya waadui, ambao watavinyanganya na kuvipeleka Babeli.