Jeremiah 20:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kwa upande wako wewe Pashuri, pamoja na nyumba yako yote, mtapelekwa utumwani; hakika mtakwenda Babuloni. Huko ndiko utakakofia na kuzikwa, kadhalika na rafiki zako wote ambao uliwatabiria uongo.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawe Pashuri pamoja na wote wanaoishi katika nyumba yako mtaenda uhamishoni Babeli. Mtafia huko na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wewe, Pashuri, na watu wote wanaokaa katika nyumba yako, mtakwenda utumwani; nawe utafika Babeli, na huko utakufa, na huko utazikwa, wewe, na rafiki zako wote, uliowatabiria maneno ya uongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kwa upande wako wewe Pashuri, pamoja na nyumba yako yote, mtapelekwa utumwani; hakika mtakwenda Babuloni. Huko ndiko utakakofia na kuzikwa, kadhalika na rafiki zako wote ambao uliwatabiria uongo.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wewe, Pashuri, na watu wote wanaokaa katika nyumba yako, mtakwenda utumwani; nawe utafika Babeli, na huko utakufa, na huko utazikwa, wewe, na rafiki zako wote, uliwatolea unabii wa uongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kwa upande wako wewe Pashuri, pamoja na nyumba yako yote, mtapelekwa utumwani; hakika mtakwenda Babuloni. Huko ndiko utakakofia na kuzikwa, kadhalika na rafiki zako wote ambao uliwatabiria uongo.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Pashuri nawe nao wote wakaao nyumbani mwako mtakwenda kwa kutekwa, utafika Babeli, utakufa huko, utazikwa huko wewe na wapenzi wako wote, uliowafumbulia maneno ya uwongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wewe, Pashuri, na watu wote wanaokaa katika nyumba yako, mtakwenda utumwani; nawe utafika Babeli, na huko utakufa, na huko utazikwa, wewe, na rafiki zako wote, uliowatabiria maneno ya uongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa upande wako, wewe Pashuri, pamoja na watu wote wanaokaa ndani ya nyumba yako, mutapelekwa katika utumwa. Hakika mutakwenda Babeli na huko ndiko utakapokufia na kuzikwa, pamoja na warafiki zako wote uliowatabiria uongo.