Jeremiah 21:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
enyi jamaa ya Daudi! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tekelezeni haki tangu asubuhi, na kuwakomboa mikononi mwa wadhalimu wote walionyanganywa mali zao. La sivyo, hasira yangu itachomoza kama moto, itawaka na wala hakuna atakayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yenu maovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi, mwokoeni mikononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara, la sivyo ghadhabu yangu italipuka na kuwaka kama moto kwa sababu ya uovu mlioufanya: itawaka na hakuna wa kuizima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee nyumba ya Daudi, Bwana asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu ye yote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
enyi jamaa ya Daudi! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tekelezeni haki tangu asubuhi, na kuwakomboa mikononi mwa wadhalimu wote walionyang'anywa mali zao. La sivyo, hasira yangu itachomoza kama moto, itawaka na wala hakuna atakayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yenu maovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo BWANA asemalo: “ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi, Mwokoeni kutoka mikononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara, la sivyo ghadhabu yangu italipuka na kuwaka kama moto kwa sababu ya uovu mlioufanya: itawaka na hakuna wa kuizima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo bwana asemalo: “ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi, mwokoeni mikononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara, la sivyo ghadhabu yangu italipuka na kuwaka kama moto kwa sababu ya uovu mlioufanya: itawaka na hakuna wa kuizima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu yeyote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
enyi jamaa ya Daudi! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tekelezeni haki tangu asubuhi, na kuwakomboa mikononi mwa wadhalimu wote walionyanganywa mali zao. La sivyo, hasira yangu itachomoza kama moto, itawaka na wala hakuna atakayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yenu maovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ninyi wa mlango wa Dawidi, asubuhi pigeni mashauri, mwaponye walionyang'anywa mkiwatoa mikononi mwa wakorofi, makali yangu yasitokee kuwa moto uwakao, asipopatikana mwenye kuuzima kwa ajili ya ubaya wa matendo yenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu ye yote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi jamaa ya Daudi, Yawe anasema hivi: Kila asubui muamue maneno kufuatana na sheria yangu, muwakomboe wote walionyanganywa mali zao toka katika mikono ya watesaji. Kama si vile, hasira yangu itawaka kama moto, wala hakuna atakayeweza kuizimisha, kwa sababu ya matendo yenu maovu.