Jeremiah 21:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tafadhali, tuombee kwa Mwenyezi-Mungu maana Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, anaanza vita dhidi yetu. Labda Mwenyezi-Mungu atatufanyia mwujiza kama afanyavyo mara kwa mara na kumfanya Nebukadneza atuache na kwenda zake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tuulizie sasa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda Mwenyezi Mungu atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tafadhali utuulizie habari kwa Bwana; kwa maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda Bwana atatutendea sawasawa na kazi zake zote za ajabu, ili aende zake akatuache.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tafadhali, tuombee kwa Mwenyezi-Mungu maana Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, anaanza vita dhidi yetu. Labda Mwenyezi-Mungu atatufanyia mwujiza kama afanyavyo mara kwa mara na kumfanya Nebukadneza atuache na kwenda zake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tuulizie sasa kwa BWANA kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda BWANA atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita ili Nebukadneza atuondokee.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tuulizie sasa kwa bwana, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda bwana atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tafadhali utuulizie habari kwa BWANA; kwa maana Nebukadneza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda BWANA atatutendea sawasawa na kazi zake zote za ajabu, na kumfanya aende zake akatuache.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tafadhali, tuombee kwa Mwenyezi-Mungu maana Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, anaanza vita dhidi yetu. Labda Mwenyezi-Mungu atatufanyia mwujiza kama afanyavyo mara kwa mara na kumfanya Nebukadneza atuache na kwenda zake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwulize Bwana kwa ajili yetu, kwani Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, ametuletea vita. Labda Bwana atatufanyizia nasi, kama mataajabu yake yote yalivyo, akiwaondoa kwetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tafadhali utuulizie habari kwa BWANA; kwa maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda BWANA atatutendea sawasawa na kazi zake zote za ajabu, ili aende zake akatuache.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tafazali, utuombee kwa Yawe, maana Nebukadneza mufalme wa Babeli anaanza kupigana vita nasi. Labda Yawe atatufanyia mumoja wa miujiza yake na kumurudisha Nebukadneza aache kutushambulia.