Jeremiah 21:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nendeni mkamwambie Sedekia kwamba hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli: “Sedekia! Nitakugeuzia wewe mwenyewe silaha unazotumia kupigana na mfalme wa Babuloni na Wakaldayo wanaowazingira nje ya kuta za mji. Nitazikusanya silaha zote katikati ya mji huu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo walio nje ya ukuta wakiwazingira kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalieni, nitazigeuza nyuma silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo kwa hizo ninyi mnapigana na mfalme wa Babeli, na Wakaldayo, wanaowahusuru nje ya kuta zenu, nami nitazikusanya pamoja katikati ya mji huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nendeni mkamwambie Sedekia kwamba hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli: “Sedekia! Nitakugeuzia wewe mwenyewe silaha unazotumia kupigana na mfalme wa Babuloni na Wakaldayo wanaowazingira nje ya kuta za mji. Nitazikusanya silaha zote katikati ya mji huu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Hili ndilo bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalieni, nitazigeuza nyuma silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo kwa hizo ninyi mnapigana na mfalme wa Babeli, na Wakaldayo, wanaowahusuru nje ya kuta zenu, nami nitazikusanya pamoja katikati ya mji huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nendeni mkamwambie Sedekia kwamba hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli: “Sedekia! Nitakugeuzia wewe mwenyewe silaha unazotumia kupigana na mfalme wa Babuloni na Wakaldayo wanaowazingira nje ya kuta za mji. Nitazikusanya silaha zote katikati ya mji huu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mtaniona, nikivirudisha vyombo vya vita vilivyo mikononi mwenu, mlivyovitumia kupiga vita na mfalme wa Babeli na Wakasidi wanaowasonga! Nitavitoa huko nje, nivilete kwenye boma, kisha nitavikusanya humu mjini katikati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalieni, nitazigeuza nyuma silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo kwa hizo ninyi mnapigana na mfalme wa Babeli, na Wakaldayo, wanaowahusuru nje ya kuta zenu, nami nitazikusanya pamoja katikati ya mji huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Zedekia, nitakugeuzia wewe mwenyewe silaha unazozitumia kwa kupigana na mufalme wa Babeli na waaskari wake wanaozunguka inje ya kuta za muji wenu. Nitazikusanya silaha zile katikati ya muji huu.