Jeremiah 21:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu atakayebaki mjini humu atauawa kwa upanga au kwa njaa au kwa maradhi mabaya. Lakini mtu atakayetoka nje ya mji na kujisalimisha kwa Wakaldayo wanaouzingira mji, ataishi; naam, atayanusurisha maisha yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayeenda na kujisalimisha kwa Wakaldayo, ambao wameuzingira mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu atakayebaki mjini humu atauawa kwa upanga au kwa njaa au kwa maradhi mabaya. Lakini mtu atakayetoka nje ya mji na kujisalimisha kwa Wakaldayo wanaouzingira mji, ataishi; naam, atayanusurisha maisha yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ye yote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini ye yote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi atanusurika, naye ataishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu atakayebaki mjini humu atauawa kwa upanga au kwa njaa au kwa maradhi mabaya. Lakini mtu atakayetoka nje ya mji na kujisalimisha kwa Wakaldayo wanaouzingira mji, ataishi; naam, atayanusurisha maisha yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Atakayekaa humu mjini atakufa kwa upanga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya. Lakini atakayetoka na kuwaangukia Wakasidi wanaowasonga atapona, nayo roho yake itakuwa pato lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu atakayebaki katika muji huu atauawa kwa vita au kwa njaa au kwa magonjwa makali. Lakini mutu atakayetoka inje ya muji huu na kujitoa kwa Wababeli wanaozunguka ukuta wake, ataishi; kweli ataokoa maisha yake.