Jeremiah 22:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ole wako Yehoyakimu wewe unayejenga nyumba kwa dhuluma na kuiwekea ghorofa bila kutumia haki. Unawaajiri watu wakutumikie bure wala huwalipi mishahara yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa dhuluma, vyumba vyake vya juu kwa udhalimu, akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo, bila kuwalipa kwa utumishi wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ole wako Yehoyakimu wewe unayejenga nyumba kwa dhuluma na kuiwekea ghorofa bila kutumia haki. Unawaajiri watu wakutumikie bure wala huwalipi mishahara yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma, vyumba vyake vya juu kwa udhalimu, akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo, bila kuwalipa kwa utumushi wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma, vyumba vyake vya juu kwa udhalimu, akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo, bila kuwalipa kwa utumishi wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ole wako Yehoyakimu wewe unayejenga nyumba kwa dhuluma na kuiwekea ghorofa bila kutumia haki. Unawaajiri watu wakutumikie bure wala huwalipi mishahara yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatampata aijengaye nyumba yake kwa njia isiyoongoka, navyo vyumba vyake vilivyomo kwa njia isiyo sawa; huzitumia kazi za mwenziwe bure tu asipompa mshahara wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole kwako Yoyakimu, wewe unayejijengea nyumba kwa njia isiyokuwa ya haki, na kuiwekea magorofi kwa njia isiyofuata sheria ya Mungu. Unayewatumikisha watu bure pasipo kuwalipa mishahara yao.