Jeremiah 22:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe wasema: ‘Nitalijenga jumba kubwa, lenye vyumba vikubwa ghorofani.’ Kisha huifanyia madirisha, ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi, na kuipaka rangi nyekundu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Anasema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme, na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’ Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa, huweka kuta za mbao za mwerezi, na kuzipaka kwa rangi nyekundu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Asemaye, Nitajijengea nyumba pana na vyumba vipana; Naye hujikatia madirisha; Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi, Na kupakwa rangi nyekundu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe wasema: ‘Nitalijenga jumba kubwa, lenye vyumba vikubwa ghorofani.’ Kisha huifanyia madirisha, ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi, na kuipaka rangi nyekundu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asemaye, ‘Nitajijengea jumba kubwa la kifalme na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’ Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa, huweka mbao za mierezi na kuipamba kwa rangi nyekundu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme, na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’ Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa, huweka kuta za mbao za mierezi, na kuipamba kwa rangi nyekundu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Asemaye, Nitajijengea nyumba kubwa yenye vyumba vipana; Naye hujikatia madirisha; Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi, Na kupakwa rangi nyekundu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe wasema: ‘Nitalijenga jumba kubwa, lenye vyumba vikubwa ghorofani.’ Kisha huifanyia madirisha, ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi, na kuipaka rangi nyekundu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Anasema: Nitajijengea nyumba kubwa yenye vyumba vipana, nitavitobolea madirisha, nitavipigilia juu mbao za miangati, kisha nitavipaka rangi nyekundu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Asemaye, Nitajijengea nyumba pana na vyumba vipana; Naye hujikatia madirisha; Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi, Na kupakwa rangi nyekundu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe unayesema: Nitajijengea nyumba kubwa, yenye vyumba vikubwa vya magorofi. Kisha unaifanyia madirisha, ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi, na kuipaka rangi nyekundu!