Jeremiah 22:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unadhani umekuwa mfalme kwa kushindana kujenga kwa mierezi? Baba yako alikula na kunywa, akatenda mambo ya haki na mema ndipo mambo yake yakamwendea vema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Je, huko kuongeza idadi ya mierezi kutakufanya uwe mfalme? Je, baba yako hakula na kunywa? Alifanya yaliyo sawa na haki, naye akafanikiwa kwa yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Utatawala kwa sababu unashindana na watu kwa mierezi? Baba yako, je! Hakula na kunywa, na kufanya hukumu na haki? Hapo ndipo alipofanikiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unadhani umekuwa mfalme kwa kushindana kujenga kwa mierezi? Baba yako alikula na kunywa, akatenda mambo ya haki na mema ndipo mambo yake yakamwendea vema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Je, inakufanya kuwa mfalme kwa kuongeza idadi ya mierezi? Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji? Alifanya yaliyo sawa na haki, hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Je, inakufanya kuwa mfalme huko kuongeza idadi ya mierezi? Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji? Alifanya yaliyo sawa na haki, hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Utatawala kwa sababu unashindana na watu kwa mierezi? Baba yako, je! Hakula na kunywa, na kufanya hukumu na haki? Hapo ndipo alipofanikiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unadhani umekuwa mfalme kwa kushindana kujenga kwa mierezi? Baba yako alikula na kunywa, akatenda mambo ya haki na mema ndipo mambo yake yakamwendea vema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Ufalme wako ni kushindana na miangati? Je? Baba yako hakula, hakunywa? Lakini amefanya yaliyo sawa yaongokayo; ndipo, alipopata kukaa vema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Utatawala kwa sababu unashindana na watu kwa mierezi? Baba yako, je! Hakula na kunywa, na kufanya hukumu na haki? Hapo ndipo alipofanikiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unazani umekuwa mufalme kwa kujenga na mierezi? Baba yako alikula na kunywa, alifuata sheria yangu na kutenda mambo ya haki, na mambo yake yaliendeka vizuri.