Jeremiah 22:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda: Wakati atakapokufa, hakuna atakayemwombolezea akisema, ‘Ole, kaka yangu!’ ‘Ole, dada yangu!’ Hakuna atakayemlilia akisema, ‘Maskini, bwana wangu!’ ‘Maskini, mfalme wangu!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: “Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, ndugu yangu! Ole, dada yangu!’ Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, Bwana asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda: Wakati atakapokufa, hakuna atakayemwombolezea akisema, ‘Ole, kaka yangu!’ ‘Ole, dada yangu!’ Hakuna atakayemlilia akisema, ‘Maskini, bwana wangu!’ ‘Maskini, mfalme wangu!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: “Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, ndugu yangu! Ole umbu langu!’ Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: “Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’ Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, BWANA asema hivi, kuhusu habari za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda: Wakati atakapokufa, hakuna atakayemwombolezea akisema, ‘Ole, kaka yangu!’ ‘Ole, dada yangu!’ Hakuna atakayemlilia akisema, ‘Maskini, bwana wangu!’ ‘Maskini, mfalme wangu!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya Yoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda: Hawatamwombolezea kwamba: A ndugu yetu! A umbu letu! Wala hawatamwombolezea kwamba: A bwana! A mwenye utukufu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, BWANA asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Yawe anasema hivi juu ya Yoyakimu mwana wa Yosia, mufalme wa Yuda: Wakati atakapokufa, hakuna atakayeomboleza juu yake, akisema: Yowe, ndugu yangu! Yowe, dada yangu! Wala hakuna atakayemulilia, akisema: Yowe, bwana wetu! Yowe, muheshimiwa wetu!