Jeremiah 22:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi wakazi wote wa Lebanoni, nyinyi mkaao salama kati ya mierezi; jinsi gani mtakavyopiga kite uchungu utakapowakumba, uchungu kama wa mama anayejifungua!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe uishiye Lebanoni, wewe uliyetulia kwenye majengo ya mwerezi, tazama jinsi utakavyoomboleza maumivu makali yatakapokupata, maumivu kama ya mwanamke mwenye uchungu wa kuzaa!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe ukaaye Lebanoni, Ufanyaye kioto chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo utungu kama wa mwanamke azaaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi wakazi wote wa Lebanoni, nyinyi mkaao salama kati ya mierezi; jinsi gani mtakavyopiga kite uchungu utakapowakumba, uchungu kama wa mama anayejifungua!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wewe uishiye Lebanoni, wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi, tazama jinsi utakavyoomboleza maumivu makali yatakapokupata, maumivu kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe uishiye Lebanoni, wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi, tazama jinsi utakavyoomboleza maumivu makali yatakapokupata, maumivu kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe ukaaye Lebanoni, Ujengaye kiota chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo uchungu kama wa mwanamke azaaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi wakazi wote wa Lebanoni, nyinyi mkaao salama kati ya mierezi; jinsi gani mtakavyopiga kite uchungu utakapowakumba, uchungu kama wa mama anayejifungua!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unakaa kama ndege ya Libanoni katika tundu kwenye miangati; lakini utapaswa na kuhurumiwa, machungu yatakapokujia yatakayokuwa kama uchungu wa mzazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe ukaaye Lebanoni, Ufanyaye kioto chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo utungu kama wa mwanamke azaaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi wakaaji wote wa Lebanoni, ninyi munaokaa salama kati ya miti ya mierezi, mutaugua sana wakati mutakaposhikwa na uchungu unaokuwa kama wa mwanamuke anayezaa!