Jeremiah 22:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kuhusu Konia mfalme wa Yuda, mwanawe Yehoyakimu, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu kwamba hata kama wewe Konia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekuvulia mbali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hakika kama niishivyo,” asema Mwenyezi Mungu, “hata kama wewe, Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekung’oa hapo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama niishivyo mimi, asema Bwana, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye muhuri katika mkono wangu wa kuume, ningekung'oa wewe hapo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kuhusu Konia mfalme wa Yuda, mwanawe Yehoyakimu, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu kwamba hata kama wewe Konia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekuvulia mbali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hakika kama niishivyo,” asema BWANA, “hata kama wewe, Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekung'oa utoke hapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hakika kama niishivyo,” asema bwana, “hata kama wewe, Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekung’oa hapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekung'oa wewe hapo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kuhusu Konia mfalme wa Yuda, mwanawe Yehoyakimu, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu kwamba hata kama wewe Konia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekuvulia mbali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, kama wewe Konia, mwana wa Yoyakimu, mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yenye muhuri mkononi pangu pa kuume, ningekuondoa kwa nguvu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye muhuri katika mkono wangu wa kuume, ningekung’oa wewe hapo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Kama vile ninavyoishi, hata kama wewe Konia mwana wa Yoyakimu, mufalme wa Yuda, ungekuwa wa lazima kwangu kama vile pete yangu ya muhuri ninayovaa kwa mukono wangu wa kuume, ningekuvua.