Jeremiah 22:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: Mwandike mtu huyu kwamba hana watoto, mtu ambaye hatafanikiwa maishani mwake. Maana hakuna hata mmoja wa wazawa wake atakayekikalia kiti cha enzi cha Daudi na kutawala tena katika Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto, mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote, kwa maana hakuna mzao wake atakayefanikiwa, wala kukaa kwenye kiti cha utawala cha Daudi wala kuendelea kutawala katika Yuda.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: Mwandike mtu huyu kwamba hana watoto, mtu ambaye hatafanikiwa maishani mwake. Maana hakuna hata mmoja wa wazawa wake atakayekikalia kiti cha enzi cha Daudi na kutawala tena katika Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA asemalo: “Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto, mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote, kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa, kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi wala kuendelea kutawala katika Yuda.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana asemalo: “Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto, mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote, kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa, wala kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi wala kuendelea kutawala katika Yuda.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: Mwandike mtu huyu kwamba hana watoto, mtu ambaye hatafanikiwa maishani mwake. Maana hakuna hata mmoja wa wazawa wake atakayekikalia kiti cha enzi cha Daudi na kutawala tena katika Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Bwana anavyosema: Mwandikeni mtu huyu kuwa pasipo watoto, kuwa mtu asiyejipatia mema siku zake zote, hata katika kizazi chake hamna mtu atakayejipatia kukikalia kiti cha kifalme cha Dawidi na kuwatawala Wayuda tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Muandike mutu huyu kwamba hana watoto, ni mutu ambaye hatafanikiwa katika maisha yake. Maana hakuna hata mumoja wa wazao wake atakayekiikalia kiti cha kifalme cha Daudi na kutawala tena katika Yuda.