Jeremiah 23:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya laana, nchi inaomboleza, na malisho ya nyanda zake yamekauka. Mienendo ya watu ni miovu, nguvu zao zinatumika isivyo halali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya laana, nchi imekauka, na malisho ya nyikani yamekauka. Mwenendo wa manabii ni mbaya na mamlaka yao si ya haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya laana, nchi inaomboleza, na malisho ya nyanda zake yamekauka. Mienendo ya watu ni miovu, nguvu zao zinatumika isivyo halali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya laana nchi imekauka na malisho yaliyoko nyikani yamekauka. Mwenendo wa manabii ni mbaya na mamlaka yao si ya haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya laana, nchi imekauka na malisho yaliyoko nyikani yamekauka. Mwenendo wa manabii ni mbaya na mamlaka yao si ya haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya laana, nchi inaomboleza, na malisho ya nyanda zake yamekauka. Mienendo ya watu ni miovu, nguvu zao zinatumika isivyo halali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nchi hii imezaa wazinzi, kwa hiyo nchi hii inakaa matanga kwa kuapizwa, mbuga za nyikani zimekauka, kwa kuwa ni mabaya, wanayoyakimbilia, nayo nguvu yao siyo ifaayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, inchi imejaa wazinzi. Kwa sababu ya laana, inchi inaomboleza, na mashamba ya kulishia nyama yamekauka. Mienendo ya watu ni miovu, wanapoteza nguvu kwa ajili ya mambo yasiokuwa ya haki.