Jeremiah 23:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini miongoni mwa manabii wa Yerusalemu, nimeona kinyaa cha kutisha zaidi: Wanafanya uzinzi na kusema uongo; wanawaunga mkono wanaotenda maovu hata pasiwe na mtu anayeachana na uovu. Kwangu wote wamekuwa kama watu wa Sodoma; wakazi wake wamekuwa wabaya kama watu wa Gomora.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu nimeona jambo baya sana: Wanafanya uzinzi na kuenenda katika uongo. Wanatia nguvu mikono ya watenda maovu, kwa ajili hiyo hakuna yeyote anayeachana na uovu wake. Wote wako kama Sodoma kwangu; watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini miongoni mwa manabii wa Yerusalemu, nimeona kinyaa cha kutisha zaidi: wanafanya uzinzi na kusema uongo; wanawaunga mkono wanaotenda maovu hata pasiwe na mtu anayeachana na uovu. Kwangu wote wamekuwa kama watu wa Sodoma; wakazi wake wamekuwa wabaya kama watu wa Gomora.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu nimeona jambo baya sana: Wanafanya uzinzi na kuenenda katika uongo. Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya, kwa ajili hiyo hakuna ye yote anayeachana na uovu wake. Wote wako kama Sodoma kwangu; watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu nimeona jambo baya sana: Wanafanya uzinzi na kuenenda katika uongo. Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya, kwa ajili hiyo hakuna yeyote anayeachana na uovu wake. Wote wako kama Sodoma kwangu; watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini miongoni mwa manabii wa Yerusalemu, nimeona kinyaa cha kutisha zaidi: Wanafanya uzinzi na kusema uongo; wanawaunga mkono wanaotenda maovu hata pasiwe na mtu anayeachana na uovu. Kwangu wote wamekuwa kama watu wa Sodoma; wakazi wake wamekuwa wabaya kama watu wa Gomora.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa wafumbuaji wa Yerusalemu nimeona mastusho: huzini, huendelea na kudanganya, huitia mikono ya wabaya nguvu, wasiuache kila mtu ubaya wake, wote pia wameniwia kama Wasodomu, nao wakaao humo kama Wagomora.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kati ya manabii wa Yerusalema, nimeona mambo ya kutisha zaidi: wao wanafanya uzinzi na kusema uongo; wanawaunga mukono wanaotenda maovu hata kusikuwe mutu anayeachana na uovu. Kwangu wote wamekuwa kama watu wa Sodoma; wakaaji wake wamekuwa kama watu wa Gomora.