Jeremiah 23:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wao hawakomi kuwaambia wale wanaodharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu: ‘Mambo yatawaendea vema.’ Na kumwambia kila mtu afuataye kwa ukaidi fikira zake; ‘Hakuna baya lolote litakalokupata!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi, ‘Mwenyezi Mungu asema: Mtakuwa na amani.’ Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao, wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daima huwaambia wao wanaonidharau, Bwana amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wo wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wao hawakomi kuwaambia wale wanaodharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu: ‘Mambo yatawaendea vema.’ Na kumwambia kila mtu afuataye kwa ukaidi fikira zake; ‘Hakuna baya lolote litakalokupata!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi kwamba, BWANA asema: ‘Mtakuwa na amani.’ Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi, ‘ bwana asema: Mtakuwa na amani.’ Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao, wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daima huwaambia wao wanaonidharau, BWANA amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wowote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wao hawakomi kuwaambia wale wanaodharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu: ‘Mambo yatawaendea vema.’ Na kumwambia kila mtu afuataye kwa ukaidi fikira zake; ‘Hakuna baya lolote litakalokupata!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huwaambia wanibezao: Bwana amesema: Mtakaa na kutengemana! Kila mtu aufuataye ushupavu wa moyo wake humwambia: Hakuna kibaya kitakachowafikia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daima huwaambia wao wanaonidharau, BWANA amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wo wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanawaambia hivi wale wanaozarau neno langu mimi Yawe: Mambo yenu yataendelea vizuri. Na wanamwambia hivi kila mutu anayefuata ugumu wa moyo wake na mawazo yake: Hakuna hasara yoyote itakayokupata!