Jeremiah 23:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, ni yupi kati ya manabii hao aliyepata kuhudhuria baraza la Mwenyezi-Mungu, hata akasikia na kuelewa neno lake? Au ni nani aliyejali neno lake, hata akapata kulitangaza?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la Mwenyezi Mungu ili kuona au kusikia neno lake? Ni nani aliyesikiliza na kusikia neno lake?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la Bwana, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, ni yupi kati ya manabii hao aliyepata kuhudhuria baraza la Mwenyezi-Mungu, hata akasikia na kuelewa neno lake? Au ni nani aliyejali neno lake, hata akapata kulitangaza?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la BWANA ili kuona au kusikia neno lake? Ni nani aliyesikiliza na kusikia neno lake?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la bwana ili kuona au kusikia neno lake? Ni nani aliyesikiliza na kusikia neno lake?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la BWANA, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, ni yupi kati ya manabii hao aliyepata kuhudhuria baraza la Mwenyezi-Mungu, hata akasikia na kuelewa neno lake? Au ni nani aliyejali neno lake, hata akapata kulitangaza?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani yuko nani aliyesimama penye njama ya Bwana, akimwona au akilisikia neno lake? Yuko nani aliyeliangalia Neno lake, akilisikia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la BWANA, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ni nani kati ya manabii hao aliyehuzuria katika baraza la Yawe, hata akasikia na kuelewa neno lake? Au ni nani aliyejali neno lake, hata akalielewa?