Jeremiah 23:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nabii aliyeota ndoto, na aitangaze ndoto yake, lakini yeye aliye na neno langu, na alitangaze kwa uaminifu. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema, makapi si sawa na ngano!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nabii aliyeota ndoto, na aitangaze ndoto yake, lakini yeye aliye na neno langu, na alitangaze kwa uaminifu. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema, makapi si sawa na ngano!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nabii aliyeota ndoto, na aitangaze ndoto yake, lakini yeye aliye na neno langu, na alitangaze kwa uaminifu. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema, makapi si sawa na ngano!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfumbuaji aliyeota na asimulie ndoto! Naye aliyelisikia Neno langu na aliseme Neno langu, lilivyo kweli! Kumvi na mpunga ziko na fungu gani lililo lao pamoja? ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nabii aliyeota ndoto, atangaze ndoto yake, lakini yule aliyefunuliwa ujumbe wangu autangaze kwa uaminifu. Kuna ulinganifu gani kati ya maganda na ngano? –Ni ujumbe wa Yawe.–