Jeremiah 23:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Mtu yeyote, awe nabii au kuhani, akikuuliza: ‘Uko wapi mzigo anaotubebesha Mwenyezi-Mungu?’ Wewe utawaambia: ‘Nyinyi ndio mzigo kwa Mwenyezi-Mungu naye atawatupa mbali.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi watu hawa, au nabii, au kuhani, watakapokuuliza, ‘Ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni nini?’ Wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio ujumbe. Nami nitawavua kama vazi, asema Mwenyezi Mungu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu hawa, au nabii au kuhani, atakapokuuliza, akisema, Mzigo wa Bwana ni nini? Ndipo utawaambia, Mzigo gani? Bwana asema, Nitawatupilia mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Mtu yeyote, awe nabii au kuhani, akikuuliza: ‘Uko wapi mzigo anaotubebesha Mwenyezi-Mungu?’ Wewe utawaambia: ‘Nyinyi ndio mzigo kwa Mwenyezi-Mungu naye atawatupa mbali.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Watu hawa, au nabii, au kuhani watakapokuuliza, ‘Mzigo wa BWANA ni nini?’ Wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio mzigo. Nami nitawavua kama vazi, asema BWANA.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wakati watu hawa, au nabii, au kuhani watakapokuuliza, ‘Mzigo wa bwana ni nini?’ wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio mzigo. Nami nitawavua kama vazi, asema bwana.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu hawa, au nabii au kuhani, atakapokuuliza, akisema, Mzigo wa BWANA ni nini? Ndipo utawaambia, Mzigo gani? BWANA asema, Nitawatupilia mbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Mtu yeyote, awe nabii au kuhani, akikuuliza: ‘Uko wapi mzigo anaotubebesha Mwenyezi-Mungu?’ Wewe utawaambia: ‘Nyinyi ndio mzigo kwa Mwenyezi-Mungu naye atawatupa mbali.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama watakuuliza walio wa ukoo huu au mfumbuaji au mtambikaji kwamba: Tamko zito la Bwana ni nini? ndipo, utakapowajibu: Hili ndilo tamko zito la Bwana, akisema: Nitawabwaga ninyi! ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu hawa, au nabii au kuhani, atakapokuuliza, akisema, Mzigo wa BWANA ni nini? Ndipo utawaambia, Mzigo gani? BWANA asema, Nitawatupilia mbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akaniambia: Mutu yeyote, akuwe nabii au kuhani akikuuliza “Uko wapi muzigo Yawe anaotubebesha?”, wewe utawaambia: Ninyi ndio muzigo kwa Yawe, naye atawatupa mbali. –Ni ujumbe wa Yawe!–