Jeremiah 23:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini jambo la ‘Mzigo wa Mwenyezi-Mungu,’ msilitaje tena. Kile anachosema binadamu ni mzigo kwake mwenyewe. Watu wanayapotosha maneno ya Mungu aliye hai, Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina ujumbe wa Mwenyezi Mungu,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mzigo wa Bwana hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya Bwana wa majeshi, Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini jambo la ‘Mzigo wa Mwenyezi-Mungu,’ msilitaje tena. Kile anachosema binadamu ni mzigo kwake mwenyewe. Watu wanayapotosha maneno ya Mungu aliye hai, Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo wa BWANA,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo wa bwana,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mzigo wa BWANA hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya BWANA wa majeshi, Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini jambo la ‘Mzigo wa Mwenyezi-Mungu,’ msilitaje tena. Kile anachosema binadamu ni mzigo kwake mwenyewe. Watu wanayapotosha maneno ya Mungu aliye hai, Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tamko zito la Bwana wasilitaje tena! Kama wanalitaja, basi, kila mtu neno lake litamgeukia kuwa tamko zito, kwani ninyi huyageuza maneno ya Mungu aliye Mwenye uzima, aliye Bwana Mwenye vikosi, Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mzigo wa BWANA hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya BWANA wa majeshi, Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini jambo la “Muzigo wa Yawe”, musilitaje tena. Neno mwanadamu analosema litakuwa muzigo kwake mwenyewe, kwa maana munageuza maneno yangu mimi Mungu Mwenye Uzima, Yawe wa majeshi, Mungu wenu.