Jeremiah 23:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bali wataapa kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa na kuwaongoza Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na kutoka nchi zote ambako aliwatawanya.’ Kisha wataishi katika nchi yao wenyewe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
bali watasema, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bali wataapa kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa na kuwaongoza Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na kutoka nchi zote ambako aliwatawanya.’ Kisha wataishi katika nchi yao wenyewe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
bali watasema, ‘Hakika kama aishivyo BWANA, aliyewatoa wazao wa Israeli katika nchi ya kaskazini na katika nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asema BWANA. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bali watasema, ‘Hakika kama bwana aishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asema bwana. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini, Aishivyo BWANA, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bali wataapa kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa na kuwaongoza Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na kutoka nchi zote ambako aliwatawanya.’ Kisha wataishi katika nchi yao wenyewe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila wataapa wakisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima aliyewaleta wazao wa mlango wa Isiraeli akiwatoa katika nchi ya upande wa kaskazini na katika nchi zote, nilikowaendesha na kuwakimbiza; ndipo, watakapokaa huku katika nchi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini, Aishivyo BWANA, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wataapa wakisema: Kama vile Yawe anavyoishi, yule aliyewaondoa na kuwaongoza Waisraeli kutoka inchi ya kaskazini na kutoka inchi zote ambapo alipowafukuza. Na halafu wataishi katika inchi yao wenyewe. –Ni ujumbe wa Yawe.