Jeremiah 24:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babuloni kuwahamisha Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wa Yuda, mafundi stadi na masonara, kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babuloni, Mwenyezi-Mungu alinionesha ono hili: Niliona vikapu viwili vya tini vimewekwa mbele ya hekalu la Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda uhamishoni Babeli na Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Mwenyezi Mungu akanionesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akanionyesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la Bwana, baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi na wafua chuma, kutoka Yerusalemu, kuwaleta Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babuloni kuwahamisha Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wa Yuda, mafundi stadi na masonara, kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babuloni, Mwenyezi-Mungu alinionesha ono hili: Niliona vikapu viwili vya tini vimewekwa mbele ya hekalu la Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli, BWANA akanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli, bwana akanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akanionesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la BWANA, baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi na wafua chuma, kutoka Yerusalemu, kuwaleta Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babuloni kuwahamisha Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wa Yuda, mafundi stadi na masonara, kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babuloni, Mwenyezi-Mungu alinionesha ono hili: Niliona vikapu viwili vya tini vimewekwa mbele ya hekalu la Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana alinionyesha, nikaona vikapu viwili vyenye kuyu, vilikuwa vimewekwa mbele ya Jumba la Bwana, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alipokuwa amekwisha kumteka Yekonia, mwana wa Yoyakimu, mfalme wa Yuda, nao wakuu wa Yuda pamoja na mafundi wa seremala na wahunzi kuwatoa Yerusalemu na kuwapeleka Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akanionyesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la BWANA, baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi na wafua chuma, kutoka Yerusalemu, kuwaleta Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilikuwa nyuma ya Nebukadneza mufalme wa Babeli kuwahamisha Yekonia mufalme wa Yuda mwana wa Yoyakimu, pamoja na wakubwa wa inchi ya Yuda na wafundi bora na wafuaji wa vyuma kutoka Yerusalema na kuwapeleka Babeli. Yawe akanionyesha vikapu viwili vya matunda ya tini vimewekwa mbele ya hekalu la Yawe.