Jeremiah 24:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Yeremia! Unaona nini?” Mimi nikamjibu: “Naona tini. Zile nzuri ni nzuri sana, na zile mbaya ni mbaya sana hata hazifai kuliwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu akaniuliza, “Je, Yeremia, unaona nini?” Nikamjibu, “Ninaona tini zilizo nzuri ni nzuri sana, lakini zilizo mbaya, ni mbaya sana zisizofaa kuliwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Bwana akaniambia, Unaona nini Yeremia? Nikasema, Naona tini; tini nzuri zilizo nzuri sana; na tini mbovu zilizo mbovu sana, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Yeremia! Unaona nini?” Mimi nikamjibu: “Naona tini. Zile nzuri ni nzuri sana, na zile mbaya ni mbaya sana hata hazifai kuliwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA akaniuliza, “Je, Yeremia unaona nini?” Nikamjibu, “Ninaona tini zile zilizo nzuri, ni nzuri sana, lakini zilizo dhaifu, ni mbaya mno zisizofaa kuliwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana akaniuliza, “Je, Yeremia, unaona nini?” Nikamjibu, “Ninaona tini zile zilizo nzuri ni nzuri sana, lakini zilizo dhaifu ni mbovu mno zisizofaa kuliwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo BWANA akaniambia, Unaona nini Yeremia? Nikasema, Naona tini; tini nzuri zilizo nzuri sana; na tini mbovu zilizo mbovu sana, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Yeremia! Unaona nini?” Mimi nikamjibu: “Naona tini. Zile nzuri ni nzuri sana, na zile mbaya ni mbaya sana hata hazifai kuliwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akaniuliza: Unaona nini, Yeremia? Nikamwambia: Kuyu; hizi kuyu nzuri ni nzuri kabisa, nazo hizi mbaya ni mbaya kabisa, haziliki kwa ubaya wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo BWANA akaniambia, Unaona nini Yeremia? Nikasema, Naona tini; tini nzuri zilizo nzuri sana; na tini mbovu zilizo mbovu sana, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe akaniuliza: Yeremia! Unaona nini? Mimi nikamujibu: Ninaona tini. Zile nzuri ni nzuri sana, na zile mbaya ni mbaya sana hata hazifai kukuliwa.