Jeremiah 24:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Kama tini hizi zilivyo nzuri, ndivyo nitakavyowaona kuwa wema watu wa Yuda ambao niliwatoa mahali hapa na kuwapeleka uhamishoni katika nchi ya Wakaldayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama zilivyo tini hizi nzuri, ndivyo nitakavyowaangalia mateka wa Yuda, niliowatoa katika mahali hapa, waende mpaka nchi ya Wakaldayo, wapate mema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Kama tini hizi zilivyo nzuri, ndivyo nitakavyowaona kuwa wema watu wa Yuda ambao niliwatoa mahali hapa na kuwapeleka uhamishoni katika nchi ya Wakaldayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama zilivyo tini hizi nzuri, ndivyo nitakavyowaangalia mateka wa Yuda, niliowatoa mahali hapa, waende mpaka nchi ya Wakaldayo, wapate mema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Kama tini hizi zilivyo nzuri, ndivyo nitakavyowaona kuwa wema watu wa Yuda ambao niliwatoa mahali hapa na kuwapeleka uhamishoni katika nchi ya Wakaldayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu wa Isiraeli: Kama hizi kuyu nzuri zinavyopendeza, ndivyo, nitakavyowatazama kwa kupendezwa Wayuda waliotekwa, niliowatuma kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakasidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama zilivyo tini hizi nzuri, ndivyo nitakavyowaangalia mateka wa Yuda, niliowatoa katika mahali hapa, waende mpaka nchi ya Wakaldayo, wapate mema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kama tini hizi zinavyokuwa nzuri, ndivyo nitakavyowaona kuwa wema watu wa Yuda ambao niliowaondoa toka nafasi hii na kuwapeleka katika uhamisho katika inchi ya Wababeli.