Jeremiah 25:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha baada ya miaka hiyo sabini kukamilika nitamwadhibu mfalme wa Babuloni pamoja na taifa hilo. Nitaiangamiza nchi hiyo ya Wakaldayo kwa sababu ya uovu wao na kuifanya nchi iwe magofu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema Bwana, kwa sababu ya uovu wao, nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha baada ya miaka hiyo sabini kukamilika nitamwadhibu mfalme wa Babuloni pamoja na taifa hilo. Nitaiangamiza nchi hiyo ya Wakaldayo kwa sababu ya uovu wao na kuifanya nchi iwe magofu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asema BWANA. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asema bwana. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema BWANA, kwa sababu ya uovu wao, na nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha baada ya miaka hiyo sabini kukamilika nitamwadhibu mfalme wa Babuloni pamoja na taifa hilo. Nitaiangamiza nchi hiyo ya Wakaldayo kwa sababu ya uovu wao na kuifanya nchi iwe magofu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Itakuwa, miaka 70 itakapopita, nitampatilizia mfalme wa Babeli na lile kabila lote mabaya yao, waliyoyafanya; hata nchi yao Wakasidi nitaigeuza kuwa peke yake tu kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema BWANA, kwa sababu ya uovu wao, nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiyo miaka makumi saba itakapopita, nitamwazibu mufalme wa Babeli pamoja na taifa lake. Nitaiangamiza inchi hiyo ya Wababeli. –Ni ujumbe wa Yawe.– Nitafanya hivyo kwa sababu ya uovu wao na kuifanya inchi ibaki mabomoko hata milele.