Jeremiah 25:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wafalme wote wa kaskazini, mbali na karibu, mmoja baada ya mwingine. Falme zote ulimwenguni zitakunywa. Na, baada ya hao wote naye mfalme wa Babuloni atakunywa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote duniani. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki atakunywa pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na mfalme wa Sheshaki
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wafalme wote wa kaskazini, mbali na karibu, mmoja baada ya mwingine. Falme zote ulimwenguni zitakunywa. Na, baada ya hao wote naye mfalme wa Babuloni atakunywa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali mmoja baada ya mwingine, yaani, falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki atakunywa pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki atakunywa pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na falme zote za dunia, zilizoko katika dunia; na mfalme wa Sheshaki atakunywa baada yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wafalme wote wa kaskazini, mbali na karibu, mmoja baada ya mwingine. Falme zote ulimwenguni zitakunywa. Na, baada ya hao wote naye mfalme wa Babuloni atakunywa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
na wafalme wote wa nchi za upande wa kaskazini, walioko karibu nao walioko mbali, kila mtu na ndugu yake; hivyo nikawanywesha wote wenye nchi za kifalme zilizoko huku ulimwenguni; lakini mfalme wa Sesaki (Babeli) atakunywa nyuma yao wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na mfalme wa Sheshaki atakunywa baada yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wafalme wote wa kaskazini, wanaokuwa mbali na karibu, mumoja kisha mwingine. Hivi nikakunywesha falme zote za ulimwengu. Na kwa mwisho naye mufalme wa Babeli akakunywa.