Jeremiah 25:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama wakikataa kukipokea kikombe hicho mkononi mwako na kunywa, wewe utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema kwamba ni lazima wanywe!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Ni lazima mnywe!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama wakikataa kukipokea kikombe hicho mkononi mwako na kunywa, wewe utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema kwamba ni lazima wanywe!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama wakikataa kukipokea kikombe hicho mkononi mwako na kunywa, wewe utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nasema kwamba ni lazima wanywe!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama wanakataa kukitwaa hicho kikombe mkononi mwako, wasikinywe, ndipo, utakapowaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Hamna budi kukinywa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama wakikataa kukipokea kikombe hicho utakachowapatia kwa kunywa, utasema hivi: Yawe wa majeshi anasema hivi: Ni lazima mukunywe!