Jeremiah 25:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama! Sasa ninaanza kuleta maafa katika mji unaoitwa kwa jina langu; je, mnadhani mnaweza kuepukana na adhabu? Hamtaachwa bila kuadhibiwa, maana ninaleta mauaji dhidi ya wakazi wote wa dunia. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta upanga dhidi ya wote wanaoishi duniani, asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama! Sasa ninaanza kuleta maafa katika mji unaoitwa kwa jina langu; je, mnadhani mnaweza kuepukana na adhabu? Hamtaachwa bila kuadhibiwa, maana ninaleta mauaji dhidi ya wakazi wote wa dunia. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asema bwana Mwenye Nguvu Zote.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama! Sasa ninaanza kuleta maafa katika mji unaoitwa kwa jina langu; je, mnadhani mnaweza kuepukana na adhabu? Hamtaachwa bila kuadhibiwa, maana ninaleta mauaji dhidi ya wakazi wote wa dunia. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mmeona, nilivyoanza kuufanyizia mabaya ule mji ulioitwa kwa Jina langu, nanyi mpone kabisa? Hamtapona, kwani upanga, ninaouita mimi, utawajia wote wakaao ulimwenguni; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa ninaanza kuleta hasara katika muji unaojulikana kwa jina langu, basi ninyi munazani kwamba munaweza kuepuka azabu? Hamutaachwa bila kuazibiwa, maana ninaleta mauaji juu ya wakaaji wote wa dunia. –Ni ujumbe wa Yawe.