Jeremiah 25:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, wewe Yeremia utatabiri maneno haya yote dhidi yao, na kusema hivi: Mwenyezi-Mungu atanguruma kutoka juu, atatoa sauti yake kutoka makao yake matakatifu; atanguruma kwa nguvu dhidi ya watu wake, na kupaza sauti kama wenye kusindika zabibu, dhidi ya wakazi wote wa dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie: “ ‘Mwenyezi Mungu atanguruma kutoka juu; atatoa sauti ya ngurumo kutoka makao yake matakatifu na kunguruma kwa nguvu sana dhidi ya nchi yake. Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu, atapiga kelele dhidi ya wote wanaoishi katika nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, tabiri wewe maneno haya yote juu yao, na kuwaambia, Bwana atanguruma toka juu, Naye atatoa sauti yake toka patakatifu pake; Atanguruma sana juu ya zizi lake; Atapiga kelele kama mtu akanyagaye zabibu, Juu ya wenyeji wote wa dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, wewe Yeremia utatabiri maneno haya yote dhidi yao, na kusema hivi: Mwenyezi-Mungu atanguruma kutoka juu, atatoa sauti yake kutoka makao yake matakatifu; atanguruma kwa nguvu dhidi ya watu wake, na kupaza sauti kama wenye kusindika zabibu, dhidi ya wakazi wote wa dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie: “ ‘BWANA atanguruma kutoka juu; atatoa sauti ya ngurumo kutoka makao yake matakatifu na kunguruma kwa nguvu sana dhidi ya nchi yake. Atapiga kelele kama wao wakanyagao mizabibu, atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie: “ ‘ bwana atanguruma kutoka juu; atatoa sauti ya ngurumo kutoka makao yake matakatifu na kunguruma kwa nguvu sana dhidi ya nchi yake. Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu, atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, tabiri wewe maneno haya yote juu yao, na kuwaambia, BWANA atanguruma toka juu, Naye atatoa sauti yake toka patakatifu pake; Atanguruma sana juu ya zizi lake; Atapiga kelele kama mtu akanyagaye zabibu, Juu ya wenyeji wote wa dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, wewe Yeremia utatabiri maneno haya yote dhidi yao, na kusema hivi: Mwenyezi-Mungu atanguruma kutoka juu, atatoa sauti yake kutoka makao yake matakatifu; atanguruma kwa nguvu dhidi ya watu wake, na kupaza sauti kama wenye kusindika zabibu, dhidi ya wakazi wote wa dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wewe utawafumbulia maneno haya yote ukiwaambia: Bwana atanguruma huko juu na kupaza sauti yake katika Kao lake takatifu akiyangurumia malisho yake; atapiga yowe kama wakamuliaji wa zabibu atakapowajia watu wote wakaao huku ulimwenguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, tabiri wewe maneno haya yote juu yao, na kuwaambia, BWANA atanguruma toka juu, Naye atatoa sauti yake toka patakatifu pake; Atanguruma sana juu ya zizi lake; Atapiga kelele kama mtu akanyagaye zabibu, Juu ya wenyeji wote wa dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wewe Yeremia utatabiri maneno haya yote juu yao, na kusema hivi: Yawe atanguruma kutoka juu, atatoa sauti yake kutoka kwenye makao yake matakatifu; atanguruma kwa nguvu kwa ajili ya watu wake, atapiga kelele kama wenye kukamua zabibu, kwa ajili ya wakaaji wote wa dunia.