Jeremiah 25:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, maafa yatalikumba taifa moja baada ya lingine, na tufani itazuka kutoka miisho ya dunia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Tazama! Maafa yanaenea kutoka taifa moja hadi jingine; tufani kubwa inainuka kutoka miisho ya dunia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, maafa yatalikumba taifa moja baada ya lingine, na tufani itazuka kutoka miisho ya dunia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Tazama! Maafa yanaenea kutoka taifa moja hadi jingine; tufani kubwa inainuka kutoka miisho ya dunia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Tazama! Maafa yanaenea kutoka taifa moja hadi jingine; tufani kubwa inainuka kutoka miisho ya dunia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, maafa yatalikumba taifa moja baada ya lingine, na tufani itazuka kutoka miisho ya dunia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mtaona, mabaya yakitoka kwa kabila moja kufikia jingine, nao upepo wenye nguvu nyingi utainuka mapeoni kwa nchi, utokee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi anasema hivi: Hasara italifikia taifa kwa taifa, na zoruba itavuma kutoka miisho ya dunia.