Jeremiah 25:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ombolezeni enyi wachungaji; lieni na kugaagaa majivuni enyi wakuu wa kundi; siku za kuchinjwa kwenu na kutawanywa zimefika; mtauawa kama kondoo madume waliochaguliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji, mjigaragaze katika majivu, ninyi viongozi wa kundi. Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia; mtaanguka na kuvunjwavunjwa kama vyombo vizuri vya udongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ombolezeni enyi wachungaji; lieni na kugaagaa majivuni enyi wakuu wa kundi; siku za kuchinjwa kwenu na kutawanywa zimefika; mtauawa kama kondoo madume waliochaguliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji, mgaegae mavumbini, ninyi viongozi wa kundi. Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia; mtaanguka na kuvunjwavunjwa kama vyombo vizuri vya udongo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji, mgaagae mavumbini, ninyi viongozi wa kundi. Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia; mtaanguka na kuvunjavunjwa kama vyombo vizuri vya udongo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ombolezeni enyi wachungaji; lieni na kugaagaa majivuni enyi wakuu wa kundi; siku za kuchinjwa kwenu na kutawanywa zimefika; mtauawa kama kondoo madume waliochaguliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pigeni makelele, ninyi wachungaji, na kulia sana! Gaagaeni mavumbini, ninyi viongozi wa makundi! Kwani siku zenu zimetimia za kuchinjwa, nami nitawaponda, mwanguke chini kama chombo kilichopendeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muomboleze, enyi wachungaji; mulie na kugaagaa katika majivu, enyi wakubwa wa kundi. Siku za kuchinjwa kwenu na kusambazwa zinakaribia. Mutauawa kama kondoo dume wanene.