Jeremiah 25:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wakawaambieni kwamba kila mmoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu na matendo yake mabaya, ili mpate kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa nyinyi na wazee wenu tangu zamani, muimiliki milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walisema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya na matendo yake maovu, ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa ninyi na baba zenu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya; uacheni uovu wa matendo yenu, mkae katika nchi ambayo Bwana aliwapa, ninyi na baba zenu, tangu zamani za kale na hata milele;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wakawaambieni kwamba kila mmoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu na matendo yake mabaya, ili mpate kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa nyinyi na wazee wenu tangu zamani, muimiliki milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakasema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka katika njia yake mbaya na matendo yake maovu ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayo BWANA aliwapa ninyi na baba zenu milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walisema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya na matendo yake maovu, ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayo bwana aliwapa ninyi na baba zenu milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya; uacheni uovu wa matendo yenu, mkae katika nchi ambayo BWANA aliwapa, ninyi na baba zenu, tangu zamani za kale na hata milele;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wakawaambieni kwamba kila mmoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu na matendo yake mabaya, ili mpate kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa nyinyi na wazee wenu tangu zamani, muimiliki milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakasema: Rudini kila mtu katika njia yake mbaya na kuyaacha matendo yenu mabaya! Ndipo, mtakapokaa katika nchi, Bwana aliyowapa ninyi na baba zenu, iwe yenu ya kale na kale kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya; uacheni uovu wa matendo yenu, mkae katika nchi ambayo BWANA aliwapa, ninyi na baba zenu, tangu zamani za kale na hata milele;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao waliwaambia hivi: Kila mumoja wenu aachane na mwenendo wake mwovu na matendo yake mabaya, kusudi mupate kuishi katika inchi ambayo Yawe amewapa ninyi na babu zenu tangu zamani kuwa urizi wenu milele.