Jeremiah 26:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakuu wa Yuda waliposikia mambo hayo, walipanda kutoka katika nyumba ya mfalme, wakaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaketi penye Lango Jipya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakuu wa Yuda waliposikia habari za mambo haya, wakatoka katika nyumba ya mfalme, wakapanda juu mpaka nyumbani kwa Bwana; wakaketi, hapo watu waingiapo katika lango jipya la nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakuu wa Yuda waliposikia mambo hayo, walipanda kutoka katika nyumba ya mfalme, wakaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaketi penye Lango Jipya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka katika jumba la kifalme wakaenda katika nyumba ya BWANA na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba ya bwana na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakuu wa Yuda waliposikia habari za mambo haya, wakatoka katika nyumba ya mfalme, wakapanda juu mpaka nyumbani kwa BWANA; wakaketi, hapo watu waingiliapo katika lango jipya la nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakuu wa Yuda waliposikia mambo hayo, walipanda kutoka katika nyumba ya mfalme, wakaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaketi penye Lango Jipya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wa Yuda walipoyasikia maneno haya wakatoka nyumbani mwa mfalme, wakapanda kwenda katika Nyumba ya Bwana, wakakaa kwenye mlango mpya wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakuu wa Yuda waliposikia habari za mambo haya, wakatoka katika nyumba ya mfalme, wakapanda juu mpaka nyumbani kwa BWANA; wakaketi, hapo watu waingiapo katika lango jipya la nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakubwa wa Yuda waliposikia mambo hayo, wakapanda kutoka kwa nyumba ya mufalme, wakaenda kwenye nyumba ya Yawe, wakaikaa kwenye mulango ulioitwa: “Mulango Mupya”.