Jeremiah 26:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo makuhani na manabii wakawaambia wakuu na watu wote: “Mtu huyu anastahili hukumu ya kifo kwa maana amehubiri dhidi ya mji huu, kama nyinyi wenyewe mlivyosikia kwa masikio yenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo hapo makuhani, na manabii, wakawaambia wakuu na watu wote, wakisema, Mtu huyu amestahili kufa, kwa sababu ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo makuhani na manabii wakawaambia wakuu na watu wote: “Mtu huyu anastahili hukumu ya kifo kwa maana amehubiri dhidi ya mji huu, kama nyinyi wenyewe mlivyosikia kwa masikio yenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mabaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo hapo makuhani, na manabii, wakawaambia wakuu na watu wote, wakisema, Mtu huyu anastahili hukumu ya kifo, kwa sababu ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo makuhani na manabii wakawaambia wakuu na watu wote: “Mtu huyu anastahili hukumu ya kifo kwa maana amehubiri dhidi ya mji huu, kama nyinyi wenyewe mlivyosikia kwa masikio yenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watambikaji na wafumbuaji wakawaambia wakuu na watu wote wa ukoo huu, wakasema: Mtu huyu anapaswa na hukumu ya kuuawa, kwani mji huu ameufumbulia maneno, kama mlivyosikia ma masikio yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo hapo makuhani, na manabii, wakawaambia wakuu na watu wote, wakisema, Mtu huyu amestahili kufa, kwa sababu ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha makuhani na manabii wakawaambia wakubwa na watu wote: Mutu huyu anastahili hukumu ya kifo, kwa maana ametabiri juu ya muji huu, kama vile ninyi wenyewe mulivyosikia kwa masikio yenu.