Jeremiah 26:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Yeremia akawaambia wakuu na watu wote: “Mwenyezi-Mungu alinituma niwatabirie mambo yote mliyosikia nikiyasema dhidi ya hekalu hili na mji huu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Mwenyezi Mungu amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote, akisema, Bwana ndiye aliyenituma kutabiri juu ya nyumba hii, na juu ya mji huu, maneno hayo yote mliyoyasikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Yeremia akawaambia wakuu na watu wote: “Mwenyezi-Mungu alinituma niwatabirie mambo yote mliyosikia nikiyasema dhidi ya hekalu hili na mji huu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “BWANA amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “ bwana amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote, akisema, BWANA ndiye aliyenituma kutabiri juu ya nyumba hii, na juu ya mji huu, maneno hayo yote mliyoyasikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Yeremia akawaambia wakuu na watu wote: “Mwenyezi-Mungu alinituma niwatabirie mambo yote mliyosikia nikiyasema dhidi ya hekalu hili na mji huu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote wa ukoo huu, akasema: Bwana amenituma kuyafumbua hayo maneno yote yatakayoijia Nyumba hii na mji huu, mliyoyasikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote, akisema, BWANA ndiye aliyenituma kutabiri juu ya nyumba hii, na juu ya mji huu, maneno hayo yote mliyoyasikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yeremia akawaambia wakubwa na watu wote: Yawe alinituma niwatabirie mambo yote muliyosikia nikisema juu ya hekalu hili na muji huu.