Jeremiah 26:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ila jueni kwa hakika kwamba mkiniua, mtakuwa mmejiletea laana nyinyi wenyewe kwa kumwaga damu isiyo na hatia, na kuuletea laana mji huu na wakazi wake. Maana, ni kweli kwamba Mwenyezi-Mungu alinituma niwaambieni mambo hayo muyasikie.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, kwa kumwaga damu isiyo na hatia, mtakuwa mmejipatia dhambi juu yenu wenyewe, juu ya mji huu, na juu ya wote wanaoishi ndani yake, kwa kuwa ni kweli Mwenyezi Mungu amenituma kwenu ili niseme maneno haya masikioni mwenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini jueni yakini ya kuwa, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli Bwana amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ila jueni kwa hakika kwamba mkiniua, mtakuwa mmejiletea laana nyinyi wenyewe kwa kumwaga damu isiyo na hatia, na kuuletea laana mji huu na wakazi wake. Maana, ni kweli kwamba Mwenyezi-Mungu alinituma niwaambieni mambo hayo muyasikie.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe, na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweli bwana amenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini jueni hakika kwamba, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ila jueni kwa hakika kwamba mkiniua, mtakuwa mmejiletea laana nyinyi wenyewe kwa kumwaga damu isiyo na hatia, na kuuletea laana mji huu na wakazi wake. Maana, ni kweli kwamba Mwenyezi-Mungu alinituma niwaambieni mambo hayo muyasikie.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini jueni hili kabisa: Ninyi mtakaponiua mtafanya, damu ya mtu asiyekosa iwajie ninyi na mji huu nao wakaao humu! Kwani Bwana amenituma kweli kwenu kuyasema maneno haya masikioni penu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini jueni yakini ya kuwa, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mujue kwa hakika kwamba mukiniua, mutakuwa mumejiletea laana ninyi wenyewe kwa kumwanga damu isiyokuwa na kosa, na kuleta laana juu ya muji huu na wakaaji wake. Maana, ni kweli kwamba Yawe alinituma niwaambie mambo hayo kusudi muyasikie.