Jeremiah 26:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani na manabii: “Mtu huyu hastahili hukumu ya kifo, kwa kuwa amesema nasi kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la Bwana Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani na manabii: “Mtu huyu hastahili hukumu ya kifo, kwa kuwa amesema nasi kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la BWANA, Mungu wetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la bwana, Mungu wetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili hukumu ya kifo; kwa maana amesema nasi katika jina la BWANA Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani na manabii: “Mtu huyu hastahili hukumu ya kifo, kwa kuwa amesema nasi kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wakuu na watu wote wa ukoo huu walipowaambia watambikaji na wafumbuaji: Mtu huyu hapaswi na hukumu ya kuuawa, kwani amesema na sisi katika Jina la Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la BWANA Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wakubwa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii: Mutu huyu hastahili hukumu ya kifo. Amesema nasi kwa jina la Yawe, Mungu wetu.