Jeremiah 26:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wakati Hezekia alipokuwa mfalme wa Yuda, Mika wa Moreshethi, aliwatangazia watu wote kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi alisema hivi: ‘Mji wa Siyoni utalimwa kama shamba mji wa Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “ ‘Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu kilichofunikwa na vichaka.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mikaya Mmorashti, alitabiri katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda; akasema na watu wote wa Yuda, ya kwamba, Bwana wa majeshi asema hivi, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wakati Hezekia alipokuwa mfalme wa Yuda, Mika wa Moreshethi, aliwatangazia watu wote kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi alisema hivi: ‘Mji wa Siyoni utalimwa kama shamba mji wa Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mika wa Moreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “ ‘Mji wa Sayuni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa lundo la kifusi cha changarawe, kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu kilichoota vichaka.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: “ ‘Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu kilichofunikwa na vichaka.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mikaya Mmorashti, alitabiri katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda; akasema na watu wote wa Yuda, ya kwamba, BWANA wa majeshi asema hivi, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wakati Hezekia alipokuwa mfalme wa Yuda, Mika wa Moreshethi, aliwatangazia watu wote kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi alisema hivi: ‘Mji wa Siyoni utalimwa kama shamba mji wa Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mika wa Moreseti alikuwa mfumbuaji siku za Hizikiya, mfalme wa Yuda, akawaambia watu wote wa Yuda kwamba: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Sioni utalimwa kuwa shamba, nao Yerusalemu utageuka kuwa machungu ya mavunjiko, nao mlima wa Nyumba ya Bwana utakuwa kilima chenye mwitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mikaya Mmorashti, alitabiri katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda; akasema na watu wote wa Yuda, ya kwamba, BWANA wa majeshi asema hivi, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku Hezekia alipokuwa mufalme wa Yuda, Mika wa Moreseti aliwatangazia watu wote kwamba Yawe wa majeshi alisema hivi: Sayuni utalimiwa kama shamba, Yerusalema utabaki mabomoko, nao mulima wa hekalu utakuwa pori.