Jeremiah 26:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walimuua Mika? La! Badala yake Hezekia alimwogopa Mwenyezi-Mungu na kuomba fadhili zake. Naye Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake ya kuwaletea balaa. Lakini sisi tuko mbioni kujiletea wenyewe maafa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha Mwenyezi Mungu na kuhitaji msaada wake? Je, Mwenyezi Mungu hakuwahurumia na kughairi maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizi ya kutisha sisi wenyewe!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha Bwana, na kumwomba Bwana awafadhili; naye Bwana akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Na sisi tungetenda mabaya makuu juu ya roho zetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walimuua Mika? La! Badala yake Hezekia alimwogopa Mwenyezi-Mungu na kuomba fadhili zake. Naye Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake ya kuwaletea balaa. Lakini sisi tuko mbioni kujiletea wenyewe maafa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine ye yote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha BWANA na kuhitaji msaada wake? Je, BWANA hakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha bwana na kuhitaji msaada wake? Je, bwana hakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha BWANA, na kumwomba BWANA awafadhili; naye BWANA akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Lakini sisi tuko karibu kujiletea maafa makuu wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walimuua Mika? La! Badala yake Hezekia alimwogopa Mwenyezi-Mungu na kuomba fadhili zake. Naye Mwenyezi-Mungu akabadili nia yake ya kuwaletea balaa. Lakini sisi tuko mbioni kujiletea wenyewe maafa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Hizikiya, mfalme wa Yuda, nao Wayuda wote walimwua? Hakumcha Bwana na kuutuliza uso wake Bwana? Naye Bwana akageuza moyo, asiwafanyizie hayo mabaya, aliyowaambia. Na sisi tufanye kibaya kilicho kikuu kama hicho, tuzikoseshe roho zetu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha BWANA, na kumwomba BWANA awafadhili; naye BWANA akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Na sisi tungetenda mabaya makuu juu ya roho zetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hezekia, mufalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda hawakumwua Mika. Hezekia alimwogopa Yawe na kuomba rehema kwake. Naye Yawe akabadilisha nia yake ya kuleta hasara aliyokusudia juu yao. Lakini sisi tuko mbio kwa kujiletea hasara wenyewe.