Jeremiah 26:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Kulikuwa na mtu mwingine pia aliyetabiri kwa jina la Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo alikuwa anaitwa Uria mwana wa Shemaya, kutoka mji wa Kiriath-yearimu. Yeye alitabiri dhidi ya mji huu na dhidi ya nchi hii kama alivyofanya Yeremia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la Mwenyezi Mungu. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, kulikuwa na mtu aliyetabiri katika jina la Bwana, Uria, mwana wa Shemaya, wa Kiriath-Yearimu; yeye naye alitabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
(Kulikuwa na mtu mwingine pia aliyetabiri kwa jina la Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo alikuwa anaitwa Uria mwana wa Shemaya, kutoka mji wa Kiriath-yearimu. Yeye alitabiri dhidi ya mji huu na dhidi ya nchi hii kama alivyofanya Yeremia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la BWANA; alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la bwana. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, kulikuwa na mtu aliyetabiri katika jina la BWANA, Uria, mwana wa Shemaya, wa Kiriath-Yearimu; yeye naye alitabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
(Kulikuwa na mtu mwingine pia aliyetabiri kwa jina la Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo alikuwa anaitwa Uria mwana wa Shemaya, kutoka mji wa Kiriath-yearimu. Yeye alitabiri dhidi ya mji huu na dhidi ya nchi hii kama alivyofanya Yeremia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na mtu mwingine aliyefumbua katika Jina la Bwana, ni Uria, mwana wa Semaya wa mji wa Kiriati-Yearimu. Naye akayafumbua yote yatakayoujia mji huu na nchi hii sawasawa kama Yeremia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, kulikuwa na mtu aliyetabiri katika jina la BWANA, Uria, mwana wa Shemaya, wa Kiriath-Yearimu; yeye naye alitabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa mutu mwingine vilevile aliyetabiri kwa jina la Yawe. Mutu huyu aliitwa Uria mwana wa Semaya, wa muji wa Kiriyati-Yearimu. Yeye alitabiri juu ya muji huu na juu ya inchi hii sawasawa na maneno yale Yeremia aliyotabiri.