Jeremiah 26:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Labda watasikiliza na kuacha njia zao mbaya. Wakifanya hivyo, huenda nikabadili nia yangu kuhusu maafa niliyonuia kuwaletea kwa sababu ya matendo yao maovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huenda watasikia na kugeuka, kisha kila mmoja kutubu na kuacha njia yake mbaya. Nami nitaghairi kuleta maafa niliyopanga kufanya dhidi yao kwa sababu ya matendo yao maovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Labda watasikiliza na kuacha njia zao mbaya. Wakifanya hivyo, huenda nikabadili nia yangu kuhusu maafa niliyonuia kuwaletea kwa sababu ya matendo yao maovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huenda watasikiliza na kila mmoja akageuka kutoka katika njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya matendo yao maovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Labda watasikiliza na kuacha njia zao mbaya. Wakifanya hivyo, huenda nikabadili nia yangu kuhusu maafa niliyonuia kuwaletea kwa sababu ya matendo yao maovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Labda watasikia, warudi kila mmoja katika njia yake mbaya, nipate kugeuza moyo kwa ajili ya mabaya, niliyoyawaza kuwafanyizia kwa matendo yao mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Labda watayasikiliza na kila mumoja wao ataacha njia yake mbaya. Wakifanya hivyo, nitabadilisha nia yangu juu ya hasara niliyokusudia kuleta juu yao kwa sababu ya matendo yao maovu.