Jeremiah 26:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi Yeremia alipomaliza kutangaza mambo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwamuru ayatangaze kwa watu wote, makuhani, manabii na watu wote walimkamata na kusema, “Utakufa!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu Mwenyezi Mungu alichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote Bwana aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi Yeremia alipomaliza kutangaza mambo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwamuru ayatangaze kwa watu wote, makuhani, manabii na watu wote walimkamata na kusema, “Utakufa!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu BWANA alichomwamuru kukisema, makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu bwana alichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote BWANA aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi Yeremia alipomaliza kutangaza mambo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwamuru ayatangaze kwa watu wote, makuhani, manabii na watu wote walimkamata na kusema, “Utakufa!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeremia alipokwisha kuyasema yote, Bwana aliyomwagiza kuwaambia watu wote wa ukoo huu, ndipo, watambikaji na wafumbuaji na watu wote wa ukoo huu walipomkamata wakisema: Sharti ufe kabisa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote BWANA aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Yeremia alipomaliza kutangaza mambo yote ambayo Yawe aliyomwamuru kutangaza kwa watu wote, makuhani, manabii na watu wote walimukamata na kusema: Wewe unapaswa kuuawa!