Jeremiah 27:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu wa taifa lolote litakalomtii mfalme wa Babuloni na kumtumikia, nitawaacha wakae nchini mwao, wailime ardhi yao na kuishi humo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa taifa lolote litainama na kuweka shingo yake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asema Mwenyezi Mungu.” ’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema Bwana; nao watailima, na kukaa ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu wa taifa lolote litakalomtii mfalme wa Babuloni na kumtumikia, nitawaacha wakae nchini mwao, wailime ardhi yao na kuishi humo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa taifa lo lote litainama na kuweka shingo yake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asema BWANA.” ’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa taifa lolote litainama na kuweka shingo lake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asema bwana.” ’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema BWANA; nao watailima, na kukaa ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu wa taifa lolote litakalomtii mfalme wa Babuloni na kumtumikia, nitawaacha wakae nchini mwao, wailime ardhi yao na kuishi humo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu wa taifa litakalotia shingo zao katika makongwa ya mfalme wa Babeli, wamtumikie, nitawatuliza katika nchi yao, wailime wakikaa kwao; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema BWANA; nao watailima, na kukaa ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu wa taifa lolote litakalobeba kwenye shingo nira mufalme wa Babeli atakayolazimisha kubeba na kumutumikia, nitawaacha wakae katika inchi yao, walime udongo na kuishi humo. –Ni ujumbe wa Yawe.