Jeremiah 27:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ya nini wewe na watu wako kufa kwa vita, njaa na maradhi? Maana, hivyo ndivyo alivyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu yatakayolipata taifa lolote litakaloacha kumtumikia mfalme wa Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni, ambazo Mwenyezi Mungu ameonya kuhusu taifa lolote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama Bwana alivyosema katika habari ya taifa lile, lisilotaka kumtumikia mfalme wa Babeli?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ya nini wewe na watu wako kufa kwa vita, njaa na maradhi? Maana, hivyo ndivyo alivyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu yatakayolipata taifa lolote litakaloacha kumtumikia mfalme wa Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni ambayo BWANA ameonya juu ya taifa lo lote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni, ambazo bwana ameonya juu ya taifa lolote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama BWANA alivyosema katika habari ya taifa lile, lisilotaka kumtumikia mfalme wa Babeli?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ya nini wewe na watu wako kufa kwa vita, njaa na maradhi? Maana, hivyo ndivyo alivyosema Mwenyezi-Mungu kuhusu yatakayolipata taifa lolote litakaloacha kumtumikia mfalme wa Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu gani mnataka kufa, wewe nao walio ukoo wako, kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya, kama Bwana alivyosema kwa ajili ya taifa litakalokataa kumtumikia mfalme wa Babeli?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama BWANA alivyosema katika habari ya taifa lile, lisilotaka kumtumikia mfalme wa Babeli?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa nini wewe na watu wako munataka kufa kwa vita, njaa na magonjwa makali? Maana, hivi ndivyo Yawe alivyosema juu ya yale yatakayolipata taifa lolote litakalokataa kumutumikia mufalme wa Babeli.