Jeremiah 27:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu anasema: ‘Mimi sikuwatuma manabii hao, bali wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, pamoja na hao manabii wanaowatabirieni uongo.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Sikuwatuma hao,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana mimi sikuwatuma, asema Bwana, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu anasema: ‘Mimi sikuwatuma manabii hao, bali wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, pamoja na hao manabii wanaowatabirieni uongo.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Sikuwatuma hao,’ asema BWANA. ‘Wanatabiri uongo kwa Jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Sikuwatuma hao,’ asema bwana. ‘Wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana mimi sikuwatuma, asema BWANA, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu anasema: ‘Mimi sikuwatuma manabii hao, bali wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, pamoja na hao manabii wanaowatabirieni uongo.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Sikuwatuma, nao hufumbua katika Jina langu yenye uwongo, kusudi niwatupe ninyi, mwangamie ninyi na wafumbuaji waliowafumbulia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana mimi sikuwatuma, asema BWANA, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi sikuwatuma manabii hao. Lakini wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo nitawafukuza, nanyi mutaangamia, pamoja na hao manabii wanaowatabiria uongo. –Ni ujumbe wa Yawe.