Jeremiah 27:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, niliwaambia makuhani na watu wote: Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Msiwasikilize manabii wenu wanaowatabiria wakisema: ‘Tazama, vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu vitarudishwa hivi karibuni kutoka Babuloni’, kwa maana wanawadanganyeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikawaambia makuhani na watu hawa wote, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba ya Mwenyezi Mungu vitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pia nalisema na makuhani, na watu wote, nikisema, Bwana asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wenu, wanaowatabiria, wakisema, Tazameni, vyombo vya nyumba ya Bwana, baada ya muda kidogo, vitaletwa tena toka Babeli; maana wanawatabiria uongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, niliwaambia makuhani na watu wote: Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Msiwasikilize manabii wenu wanaowatabiria wakisema: ‘Tazama, vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu vitarudishwa hivi karibuni kutoka Babuloni’, kwa maana wanawadanganyeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikawaambia makuhani na watu wote hawa, “Hili ndilo asemalo BWANA: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba ya BWANA vitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikawaambia makuhani na watu hawa wote, “Hili ndilo asemalo bwana: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba ya bwana vitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pia nilisema na makuhani, na watu wote, nikisema, BWANA asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wenu, wanaowatabiria, wakisema, Tazameni, vyombo vya nyumba ya BWANA, baada ya muda kidogo, vitaletwa tena toka Babeli; maana wanawatabiria uongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, niliwaambia makuhani na watu wote: Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Msiwasikilize manabii wenu wanaowatabiria wakisema: ‘Tazama, vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu vitarudishwa hivi karibuni kutoka Babuloni’, kwa maana wanawadanganyeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watambikaji na watu wote wa ukoo huu nikawaambia kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msiyasikie maneno ya wafumbuaji wenu wanaowafumbulia kwamba: Mtaona, vyombo vya Nyumba ya Bwana vikirudishwa toka Babeli sasa bado kidogo tu! Kwani hao huwafumbulia yenye uwongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pia nalisema na makuhani, na watu wote, nikisema, BWANA asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wenu, wanaowatabiria, wakisema, Tazameni, vyombo vya nyumba ya BWANA, baada ya muda kidogo, vitaletwa tena toka Babeli; maana wanawatabiria uongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Yeremia akawaambia makuhani na watu wote: Yawe anasema hivi: Musiwasikilize manabii wenu wanaowatabiria, wakisema: “Vyombo vya nyumba ya Yawe vinakaribia kurudishwa kutoka Babeli,” kwa maana wanawadanganya ninyi.