Jeremiah 27:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi juu ya nguzo, sinia za shaba, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo vinavyoweza kuhamishwa, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari za nguzo, na katika habari za bahari, na katika habari za matako yake, na katika habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi juu ya nguzo, sinia za shaba, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA wa majeshi asema hivi, kuhusu habari za nguzo, na kuhusu habari za bahari, na kuhusu habari za vilingo vyake, na kuhusu habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi juu ya nguzo, sinia za shaba, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema kwa ajili yao: Zile nguzo na bahari na vilingo na vyombo vyote vilivyosalia humu mjini,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA wa majeshi asema hivi, katika habari za nguzo, na katika habari za bahari, na katika habari za matako yake, na katika habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Yawe wa majeshi anasema hivi juu ya nguzo, birika la shaba na misingi ya kuliwekea, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika muji huu,