Jeremiah 27:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vyombo hivyo vitachukuliwa Babuloni na vitabaki huko mpaka siku nitakapovishughulikia. Hapo ndipo nitakapovirudisha na kuviweka tena mahali hapa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, na huko vitabaki hadi siku nitakayovijilia,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha mahali hapa.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijilia, asema Bwana; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vyombo hivyo vitachukuliwa Babuloni na vitabaki huko mpaka siku nitakapovishughulikia. Hapo ndipo nitakapovirudisha na kuviweka tena mahali hapa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, nako huko vitabaki mpaka siku nitakayovijilia,’ asema BWANA. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha tena mahali hapa.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, nako huko vitabaki mpaka siku nitakayovijilia,’ asema bwana. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha mahali hapa.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijia, asema BWANA; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vyombo hivyo vitachukuliwa Babuloni na vitabaki huko mpaka siku nitakapovishughulikia. Hapo ndipo nitakapovirudisha na kuviweka tena mahali hapa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vitapelekwa Babeli; ndiko, vitakakokuwa mpaka siku ile, nitakapowapatiliza; ndivyo, asemavyo Bwana. Ndipo, mtakapovileta huku na kuvirudisha mahali hapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijilia, asema BWANA; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vyombo hivyo vitapelekwa Babeli, navyo vitabaki huko mpaka siku nitakapovishugulikia. Hapo ndipo nitakapovirudisha na kuviweka tena pahali hapa. –Ni ujumbe wa Yawe.