Jeremiah 27:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi ndimi niliyeiumba dunia, watu na wanyama waliomo kwa uwezo wangu na kwa mkono wangu wenye nguvu, nami humpa mtu yeyote kama nionavyo mimi kuwa sawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooka nimeumba dunia na watu wake na wanyama walio ndani yake, nami humpa yeyote ninayependa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi ndimi niliyeiumba dunia, watu na wanyama waliomo kwa uwezo wangu na kwa mkono wangu wenye nguvu, nami humpa mtu yeyote kama nionavyo mimi kuwa sawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa ye yote inipendezavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa yeyote inipendezavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio katika nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi ndimi niliyeiumba dunia, watu na wanyama waliomo kwa uwezo wangu na kwa mkono wangu wenye nguvu, nami humpa mtu yeyote kama nionavyo mimi kuwa sawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nilizifanya nchi na watu na nyama wa porini walioko katika nchi kwa nguvu yangu iliyo kuu na kwa mkono wangu uliokunjuka, nikampa anyokaye machoni pangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni mimi niliyeumba dunia, watu na nyama wanaokuwa ndani yake kwa uwezo wangu na kwa nguvu zangu kubwa. Nami ninaitoa kwa yeyote ninayetaka.