Jeremiah 27:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mataifa yote yatamtumikia yeye, mwanawe na mjukuu wake, mpaka wakati nchi yake itakapoanguka. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamfanya kuwa mtumwa wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mataifa yote yatamtumikia yeye, pamoja na mwanawe, na mjukuu wake, hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mataifa yote yatamtumikia yeye, mwanawe na mjukuu wake, mpaka wakati nchi yake itakapoanguka. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamfanya kuwa mtumwa wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mataifa yote yatamtumikia yeye pamoja na mwanawe na mwana wa mwanawe hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mataifa yote yatamtumikia yeye, pamoja na mwanawe na mwana wa mwanawe, hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mataifa yote yatamtumikia yeye, mwanawe na mjukuu wake, mpaka wakati nchi yake itakapoanguka. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamfanya kuwa mtumwa wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mataifa yote yatamtumikia yeye na mwanawe na mjukuu wake, mpaka zitakapotimia siku za nchi yake; ndipo, mataifa yenye watu wengi na wafalme wakuu watakapomtumikisha naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mataifa yote yatamutumikia yeye, pamoja na mwana wake na mujukuu wake mpaka wakati inchi yake itakapoanguka. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi wakubwa watamufanya kuwa mutumwa wao.